MZEE NJEMBA ATOWEKA NYUMBANI KWAKE , NDUGU WANAMTAFUTA.

0
326
Ndugu na jamaa
wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim “Njemba” (pichani)  ametoweka nyumbani kwake
Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya
Alhamisi tarehe 24/12/2015. 
Alionekana mara ya mwisho
kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa
kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu
na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa
hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba
mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za
dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.

NO COMMENTS