MWANAMUZIKI DENNIS EDWARD AFARIKI DUNIA

0
61


Mwimbaji mwandamizi wa kundi maarufu la Temptations Dennis Edwards amefariki dunia mwishoni mwa juma akiwa na umri wa miaka 74. Dennis alianza kuimba akiwa na umri mdogo tu wa miaka mitatu na baba yake kwenye kwaya ya kanisa na baadaye aliingia kwenye uimbaji wa nyimbo za kawaida na kujiunga na kampuni maarufu ya Motown katika bendi ya Contour 1960 kabla ya kujiunga na kundi maarufu la Temptations 1962 na ilipofika mwaka 1968 aliombwa kuchukua uongozi wa bendi hiyo baada ya aliyekuwa akiongoza kundi hilo David Ruffin kuondoka.
Na baada tu ya kuichukua uongozi wa bendi hiyo hatimaye ilishinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy 1968.Dennis atakumbukwa sana na kibao chake kilichotamba Don’t look any further.Bofya hapa kwa wimbo huo.

Aliacha na kundi la Temptation mwaka 1977 na kuamua kuimba peke yake au solo na alitamba sana na kibao chake Don’t Look any Further kilichotoka 1984 aliimba akishirikiana na Siedah Garrett.
Dennis Edwards alifunga ndoa na Ruth Pointer, mwimbaji wa kundi la Pointer sisters na baadaye kuachana naye ameacha watoto 6 wasichana 5 na mvulana mmoja.
VOA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY