Wednesday, February 21, 2018
Muhammad Buhari ndiye rais mpya wa Nigeria

Muhammad Buhari ndiye rais mpya wa Nigeria

0
353

Buhari

Pichani ni Jenerali Muhammadu Buhari akiwa katika wakati wa kampeni muda mfupi kabla ya kupiga kura.

Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan mamlakani.

Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha mpigia simu mpinzani wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.

Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung’olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.

eb81c8a72a4840e3ad7553e9388d0e61_18

Pichani ni Jenerali Muhammadu Buhari akihutubia kwenye kampeni

Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.

Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.

Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo .

150120133956_buhari_kano_640x360_ap_nocredit

Baadhi ya wafuasi wa Buhari wakiwa mitaani muda mfupi wakati wa kampeni mwishoni mwa wiki.

Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza kuing’oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.

Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.

source/Chanzo BBC SWAHILI.

NO COMMENTS