Mugabe bado ngangali atangaza kugombea tena

0
429

Rais Robert Mugabe atangaza kugombea tena mwakani.

Chama tawala cha Zimbabwe cha ZANU PF kimenza mkuitano wake Ijumaa na kinategemea kupitisha mpango wa rais Robert Mugabe kufanya uchaguzi kati kati ya mwaka ujao.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) chama hicho kinategemea kumchagua Mugabe kama mgombea wake.

Mapema mwezi huu Bw. Mugabe aliliambia gazeti la Sunday Mail kuwa serikali ya umoja ya Zimbabwe haina uhalali kamili na kwamba hapendi kuwa sehemu ya serikali hiyo.

NO COMMENTS