MSAFARA WA MAGUFULI WAPATA AJALI.

0
7567

IMG-20160206-WA0144Askari watatuwa jeshi la polisi Mkoani Singida wamefaariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenye msafara wa Rais,Dk.John Pombe Magufuli kutoka Singida kuelekea Mkoani Dodoma kupata ajali.

Aidha Dk.Magufuli pamoja na msafara wake huo walikuwa wakitokea Mjini Singida kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyoadhimishwa kitaifa Mkoani Singida walipokuwa wakirudi Mkoani Dodoma.

Ajali hiyo mbaya imetokea leo (06/2/2016) saa 9.40 alasiri katika eneo la Kijiji cha Isuna,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na kisha dereva kushindwa kulimudu.

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka waliofariki ni pamoja na Mkaguzi wa polisi,Bwana Mwanjelo,Sajenti Elias Mrope na sajenti Gerard na kwamba waliojeruhiwa ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Singida (RCO ) Bwana Peter Majira na Pc Charles,ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Amefafanua kamanda Sedoyeka kwamba kwa sasa bado taratibu za mazishi hazijaanza kuchukuliwa ambapo miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa mjini Singida.

NO COMMENTS