Sunday, February 18, 2018
Mkutano wa Takwimu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wafanyika...

Mkutano wa Takwimu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wafanyika jijini Dar Es Salaam

0
441

NBS - 1

Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kutoka Tanzania  Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu jana jijini Dar es salaam.
NBS -2
Mkurugenzi Mkuu w aOfisi ya Takwimu Rwanda  Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jana jijini Dar es salaam.
NBS-3
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Kenya Bw.  Zachary Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
NBS - 4
Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi yaTakwimu mbalimbali.
NBS -5
Mwakilishiwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi yaTakwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri akichangia wakatiwa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
NBS - 7
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Takwimu wa nchi Wanachama wa Jumuiya yaAfrika Mashariki wakifuatilia mausuala mbalimbali wakati wa Mkutano huo jana jijini Dar es salaam. (Picha na Veronica Kazimoto).

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Wakurugenzi Wakuu wa Ofisi za Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania wamekutana leo  jijini Dar es salaam kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Akifungua Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine unazileta pamoja Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Takwimu na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi hizo.

Amesema kuwa mkutano huo umelenga kuongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo katika matumizi ya Takwimu pamoja na kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya Takwimu kwa Nchi Wanachama.

Kwa upande wao wakurugenzi hao kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, na Burundi wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa matumaini ya mwendelezo wa ushirikiano katika matumizi ya takwimu sahihi kutokana na mchango wake katika maendeleo ya nchi zao na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wamesema kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi mzuri wa takwimu mbalimbali zikiwemo za kilimo, Viwanda, Biashara, uchumi  na takwimu nyingine kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.

Kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ambao umehusisha wakurugenzi wakuu, wakurugenzi na maafisa wandamizi wa takwimu ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali inayofanyika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

NO COMMENTS