Mkutano Mkuu wa Kuifufua upya Jumuiya ya watanzania DMV

0
115

Watanzania waishio Washington DC na Vitongoji vyake, siku ya Jumapili Jan 14, waliweza kufanya maamuzi ya kuifufua tena Jumuiya ya Watanzania DMV, ambayo ilivunjika kwa zaidi ya miaka miwili hadi kufikia kufanya maamuzi ya kuifufua tena upya.

Kamati ya Maandalizi pamoja na watanzania waliohudhuria katika mkutano huo, waliweza kufanya maamuzi ya kuteuwa watu saba kuwa ndani ya Kamati ya Uchaguzi, ili kufanikisha uchaguzi wa viongozi wapya watakaojitokeza kuchukua fomu za kugombea uongozi wa Jumuiya hiyo.

Viongozi wa Kamati ya muda ya Uchaguzi waliochaguliwa na Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo ni Robert Saulanga – Mwenyekiti Richard Mawenya – M/Kiti Msaidizi Julius Manase – Katibu Eddha Ghachuma – Muweka Hazina Mama Mushala – Mjumbe Kenyatta – Mjumbe Simba Sakapala.

NO COMMENTS