Mkurugenzi Muwsa ,Mhandisi Cyprian Luhemeja awaaga wafanyakazi.

0
584
Aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi
na usafi wa Mazingira mjini Moshu (MUWSA) mhandisi Cyprian Luhemeja
akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa
kauli ya kuwaaga baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Mtendaji mkuu
 DAWASCO.
Kauli ya Mhandisi Luhemeja ya kuwaaga
wafanyakazi hao ilionekana kama mwiba na kuzua simanzi kuu kwa
watumishi hao waliofanya kazi na mkurugenzi huyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja na miezi 10.
Mhandisi Luhemeja akijaribu kuwapatia
wafanyakazi hao Lugha nzuri angalau wasibaki na
majonzi.
Meneja Fedha wa MUWSA ,Joyce Msiru
akizungumza jambo katika kikao hicho.
Hali ya huzuni ndio ilitawala katika viunga
vya ofisi za Mamlaka hiyo.

Na Dixon Busagaga a Globu ya
Jamii Kanda ya Kaskazini.

NO COMMENTS