Miss Universe 2010 atokea Mexico

0
656
Miss Universe Jemina Navarrete
Miss Universe Jemina Navarrete
Miss Universe katika vazi la kuogelea
Miss Universe katika vazi la kuogelea

Mwanadada mrembo wa Mexico Jimena Navarrete ndiye ameibuka mshindi wa Miss Universe 2010 huko Las Vegas Nevada baada ya kuwatoa washiriki wengine kutoka nchi 82 duniani.

Kimwana huyo mwananana mwenye umri wa miaka 22 alishinda kwenye kinyang’anyiro cha mavazi ya kuogelea na vazi la jioni. Mrembo huyu alijipatia pointi nyingi katika kipindi cha maswali baada ya kujibu vyema swali kuhusu  wazazi wanaowaachia watoto kutumia mtandao bila  usimamizi wowote. Dada huyu alijibu kwa kupitia mkalimani kwamba mtandao ni chombo muhimu sana kwa sasa na hakiwezi kuachwa lazima tuhakikishe tunawafundisha maadili tuliyojifunza kama familia.

Majibu haya yalimpa nafasi kimwana huyu amnbaye alikuwa nyuma ya kimwana wa Phillipines ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya ushindi lakini alijikuta akiishia nafasi ya nne baada ya kushindwa kujibu vyema swali aliloulizwa. Swali lilikuwa ni kuhusu makosa gani aliyofanya maishamni mwake lakini aliishia kucheka na kusema Asante kwa nafasi hii na sikumbuki makosa yeyote maishani mwangu.

Rais wa Mexico Felipe Calderon alituma salam za pongezi kwa mrembo huyo wa nchi yake kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yake. Miss Mexico Jemina Navarrete amechukua taji kutoka kwa Stefania Fernandez Miss Venezuela ambaye alikuwa mshindi wa 2009.

Mshindi huyu wa Miss Universe atapata makazi katika nyumba ya fahari New York ambayo analipiwa kwa mwaka mzima, mshahara ambao haujatajwa, gharama zake zote zinalipwa, vito vya thamani, nguo na viatu kwa mwaka mzima na scholarship ya masomo huko New York Film Academy pamoja na malazi mara baada ya muda wake kumalizika.

Mashindano haya yanaandaliwa kwa pamoja kati ya Donald Trump na NBC TV. Chanzo cha habari yahoo!news

Miss Universe katika vazi la jioni
Miss Universe katika vazi la jioni
Miss Universe katika pozi
Miss Universe katika pozi

NO COMMENTS