Miss Tanzania 2014-15 kukabidhiwa bendera ya taifa namkuu wa mkoa wa Dar..

0
771

Miss TanzaniaMrembo wa Taifa Miss Tanzania Lilian Deus Kamazima amekabidhiwa Bendera ya Taifa na Mkuu wa Mkoa wa DSM ikiwa ni ishara ya kumtakia kila la heri katika mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika Sanya China tarehe 19 Desemba 2015.

Mrembo huyo ameondoka nchini Ijumaa tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na warembo wengine kutoka nchi zaidi ya 120 duniani na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika Hotel ya Beauty Crown Sanya China.

Miss Tanzania Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014.

Pamoja na mambo mengine ameshiriki Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda mwezi Novemba 2014.

Ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na D’salaam.

Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT Miss Tanzania Lilian anaondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.

Mrembo huyo anatarajia kurejea nchini tarehe 20 Desemba 2015.

Imetolewa na.

HIDAN .O. RICCO.
AFISA HABARI.
LINO INTERNATIONAL AGENCY LTD
0755 019288

NO COMMENTS