Miss Tanaia na Miss Kenya watembelea watoto wagonjwa .

0
564

IMG_9315

IMG_9318MISS KENYA 2014/5 IDAH NGUMA PAMOJA NA MISS TANZANIA 2014/5 LILIAN KAMAZIMA, Alhamisi walifanya ziara ya kijamii kwa kutembelea Hospital ya CCBRT wodi ya watoto wenye matatizo ya Midomo wazi, pamoja na akina mama wenye matatizo ya Fistura.

Ziara hii imedhaminiwa na Shirika la SMILE TRAIN, lililopo Nairobi Kenya ambayo mrembo wa Kenya Idah Nguma ni Balozi wa Shirika hilo.

Shirika la Smile Train linadhamini Hospital kadhaa hapa nchini pamoja na nchi za Afrika ya Mashariki kwa wagonjwa wenye matatizo hayo kutibiwa bure bila ya malipo yeyote.

Mrembo huyo kutoka Kenya ametembelea pia Uganda, na baada ya kumalizika ziara yake ya siku 2 hapa nchini Tanzania ataelekea Addis Ababa Ethiopia kwa shughuli hizo hizo za kuhamasisha akina mama kujitokeza na kupeleka watoto wao wenye matatizo kama hayo hospitalini.

NO COMMENTS

  1. Jamani hongereni sana warembo kwa maana maandiko yanasema ni heri wenye moy safi maana wao watauona ufalme wa mbinguni