MILIMA YA RORYA MKOANI MARA

0
402
Na BMG
Ni muonekano wa milima ambayo inapatikana katika Wilaya ya
Rorya mkoani Mara, Mita chache Kutoka Mto Mara ukiwa unatoka au unaelekea wilayani
Tarime, ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma-Tarime.
Maajabu ya milima ambayo iko pande zote mbili za barabara si
kwamba yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli
hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba na
kufanya abiria kuhisi uumbaji wa Mungu uliotukuka katika hii dunia.
Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katikakati ya
milima hii huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika
milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala la
mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mtelemko huwa ni mtelemko kweli
kwani ikiwa wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje japo ukweli ni kwamba
ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika milima hiyo.
Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu zisiiathiri milima
hii (mfano katika picha) maana ni tegemeo kwa wanamara na sote twajua umuhimu
wa milima kama hii ambayo ina uwepo mkubwa wa mistu ya asili.

Tazama HAPA Picha Zaidi

NO COMMENTS