Matokeo ya michezo ya NBA

0
490

Russel Brook wa Oklahoma amuuumbua Rajo Rondo wa Celtics
Michezo ya mpira wa kikapu ya Ijumaa jioni Oklahoma City Thunders wamefanya maajabu baada ya kuimwaga Boston Celtics kwa jumla ya pointi 89-84, katika mchezo huo Oklahoma hawakutegemewa kushinda ugenini hasa bila ya nyota wao Kevin Durant lakini ama kwa hakika walionyesha ujasiri wa hali ya juu na kushinda mechi hiyo.

Huku wakiongozwa na kijana chipukizi Russell Brooks aliyeweka nyavuni pointi 31.

Nao Miami Heat wakiongozwa na Lebron James walikuwa na wakati mgumu mbele ya Charlotte Bob Cats lakini hatimaye walipata ushindi baada ya kuwa nyuma kwa pointi 82-80 katika kota ya nne walrudi na kupata ushindi..

Alikuwa ni Lebron James ambaye aliongoza timu yake kwa kupachika pointi 32 akishirikiana na Chris Bosh waliofanikisha ushindi huo na Duane Wade ambaye alikuwa akiumwa kwahiyo hakuweza kufunga pointi nyingi. Mpaka mwisho wa mchezo Miami Heat waliibuka wababe kwa jumla ya pointi 95-87.

Na katika michezo mingine ya Ijumaa watoto wa nyumbani Washington Wizards wakiongozwa na Gilbert Arenas waliifunga Memphis Grizzlies 89-86 huku Grizzlies timu anayocheza mtanzania Hasheem Thabeet wakiwa wamepoteza mchezo wao watano mfululizo wakati huu ulikuwa ni ushindi wa nne mfululizo kwa Washington Wizards.

Nao Dallas Mavericks waliumbuliwa nyumbani kwao na Chicago Bulls lakini uchezaji mbaya wa safu ya ulinzi almanusura iwakoseshe Chicago ushindi baada ya Jason Terry kupiga pointi tatu zikiwa zimebaki sekunde 6 kumalizika kwa mchezo huo lakini Chicago walirudi na kupata ushindi 88-83 nje ya nyumbani kwao Derrick Rose alimaliza na plasta puani lakini alicheza kishujaa mpaka mwisho na ikiwa wakati fulani walikuwa nyuma kwa pointi 12 lakini walibadili mchezo na kurudi upya na kupata ushindi.

Katika michezo mingine ya Ijumaa Philadelphia 76ers iliwaangusha Milwaukee Bucks 90-79. Toronto iliiangusha Houston 106-96, Cleveland ilipigwa mweleka na New Orleans 108-101 wakati LA Lakers iliendeleza ubabe dhidi ya Minnesota Timberwolves 112-95, San Antonio Spurs iliifunga Utah Jazz 94-82, wakati Sacramento walitoka kifua mbele dhidi ya New Jersey 86-81.Na New York walitamba mbele ya Golden State kwa pointi 125-119.

NO COMMENTS