Mashambulizi ya kigaidi watu 37 wameuawa hotelini Tunisia .

0
337

150626124129_tunisia_attck_march_624x351_gettyMaafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.

Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
150615072514_tunisia_2_640x360_afp_nocreditPolisi wa Tunisia.

Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.

Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.
Watu 27 wameuawa hotelini Tunisia

Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.

October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
Chanzo:BBC

NO COMMENTS