Mary J athibitisha elimu haina umri

0
548

Mkongwe  wa muziki wa R&B Mary J Blidge alithibitisha kwamba elimu haina kikomo mwisho pale alipoamua kujiunga na chuo kikuu cha Howard hapa Washington Dc.

Mary J atakuwa mwanafunzi maarufu na tajiri kuliko wote katika chuo hicho maarufu cha wanafunzi weusi.

Ni chuo cha kihistoria na sasa kitaandika historia ya kuwa na mwanafunzi huyo  wa aina yake.

Prodyuza maarufu wa Sauti ya Amerika Dwayne Wade ameeleza kuwa itabidi maisha ya wanafunzi wa chuo hicho yabadilike kwa kiasi fulani ili kueza kukaa na supa staa huyo kati kati yao na itambidi awe na ulinzi wake wa kutosha kwani chuo hicho kilicho kati kati ya jiji la DC kitavamiwa na mapaparazi.

Mary J Blidge

Nalo jiji la DC lililojaa klabu za muziki za kila aina linangoja kwa hamu kubwa ujio huu wa Malkia huyu mkongwe wa hiphop na R&B.

NO COMMENTS