Marekani yamwekea vikwazo mshirika wa Mugabe

0
327

Rais Robert Mugabe

Marekani imemwekea vikwazo mwanasheria mkuu wa Zimbabwe na kusema vitendo vyake vinadharau taasisi za kidemokrasia nchini humo.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) wizara ya fedha Marekani leo imemshutumu Johannes Tomana mshirika wa rais Robert Mugabe kwa kuwalenga wapinzani fulani kwa ajili ya kuwatesa. Imesema hatua zake zinatishia utawala wa sheria nchini Zimbabwe na kuleta utete kwenye serikali yao ya ushirikiano.

Vikwazo hivyo vina maana raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara na Tomana na kwamba mali zake zilizoko Marekani zinazuiwa. Wakati huo huo mzee Mugabe ambaye anakaribia miaka 89 ametangaza kuwa ndiye mgombea wa kiti cha urais kwa chama chake cha ZANU PF mwakani.

NO COMMENTS