Mapigano yapamba moto Somalia

0
334

Maafisa wa afya katika mji mkuu wa Somalia wanasema watu wapatao 13 wameuwawa katika siku mbili za mapigano kati ya wanamgambo wa kiislam na majeshi yanayounga mkono serikali.

Kwa mujibu wa VOA Ripoti kutoka Mogadishu zinasema mapigano yalianza wakati wanamgambo wa Al shabab waliposhambulia barabara muhimu inayounganisha jumba la rais na uwanja wa ndege.

Hata hivyo, AFP imesema mmoja wa wabunge amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kuwa ni kosa kwa bunge kuliidhinisha baraza jipya la mawaziri kwani wengi wa walioteuliwa hawako nchini Somalia jambo ambalo anasema ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Waziri Mkuu mpya wa Somalia alichaguliwa baada ya kujiuzulu mtangulizi wake Abdirashid Ali Sharmake mwezi uliopita.

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991 na hadi sasa hakuna matumaini ya mapigano hayo kumalizika.

NO COMMENTS