Maandamano dhidi ya rais mteule Trump yafanyika Marekani

0
593

7eaa9d8d-285a-4144-8c36-f3074f5215ae_w987_r1_sMaandamano ya kumpiga rais mteule wa marekani Donald Trump yanafanyika katika karibu miji saba ya Marekani siku moja tu baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi ulokua na ushindani mkubwa katika historia ya karibuni ya taifa hili.

Maelfu ya watu wanaandamana New York, Chicago, Washington na miji mingine mitano Jumatano usiku ili kupinga kauli za kudhalilisha za rais mteule Trump aliyokua anatoa wakati wa kipndi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Wengi wamekua na mabango yanayolaani matamshi yake ya kuwapinga wahamiaji, waislamu na makundi mengine mbali mbali.

Akitoa hotuba yake ya kukubali ushindi Jumanne usiku huko New York, Trump alitoa wito kwa taifa kuungana na kufanya kazi pamoja.

“Sasa ni wakati kwa wamarekani kutibu majeraha ya mgawanyiko na tunabidi kuungana tena. Kwa warepublican, wademokrat na wasioegemea upande wowote kote nchini ninasema wakati umefika kwetu sisi kuungana na kuwa watu wa pamoja.”

Wito huo unaonekana haujakubaliwa na Wamarekani wote kwani Jumatano usiku waandamanaji walikusanyika pia mbele ya White House wakitoa wito wa kukomeshwa ubaguzi wakati Trump anajitayarisha kuchukua madaraka ya nchi hii.

Mapema Jumatano, Rais Barack Obama akizungmza Ikulu, alitangaza kwamba amekaribisha Trump Alhamisi huko Ikulu ili kuanza kujadili kipindi cha mpito na kukabidhiana madaraka kama ilivyo utamaduni wa demokrasia ya Marekani na kutoa wito kwa wamarekani kuungana pamoja nyuma ya rais wa 45.

“Kwa hivyo nimeagizia timu yangu kufuata mfano wa timu ya rais Bush miaka minane iliyopita na kufanya kazi kwa bidi kuhakikisha kipindi cha mpito cha rais mteule kinafanikiwa kwa sababu sisi sote tunamtakia ufanisi katika kutuunganisha na kuiongoza nchi hii.”

Maneneo hayo ya umoja yalitolewa pia naHillary Clinton wakati wa asubuhi baada ya kukubali kushindwa.

Clinton alisema taifa limegawika lakini bado anaimani na na misingi ya Marekani na hivi sasa watu wakubali kwamba Trump ndiye rais wa taifa hilo kuu.

Matamshi hayo yote yanaonekana hayakuwaridhisha baadhi ya wamarekani wenye hasira kwani walishuka mitaana kuandamana dhidi ya ushindi huo ambao haukutazamiwa.

NO COMMENTS