Maafisa wa Ufaransa wateguwa shambulizi jengine la kigaidi.

0
496

Paris Terror Attacks, November 13th 2016 - Islamic State claims responsibility for a series of mass shootings and suicide bombings that killed 128 people at least, in Le Bataclan Theatre, Le Stade de France and other locations. President Hollande declared a state of emergency – dvdbash.com
Paris Terror Attacks, November 13th 2016 – Islamic State claims responsibility for a series of mass shootings and suicide bombings that killed 128 people at least, in Le Bataclan Theatre, Le Stade de France and other locations. President Hollande declared a state of emergency – dvdbash.com
Maafisa wa usalama nchini Ufaransa wanasema wamezuiya shambulizi lililopangwa kutekelezwa kwenye msako mapema jumatano mjini Paris lakini wanaume wawili wanaosakwa kutokana na shambulizi la wiki iliopita kwenye mji mkuu wa Ufaransa sio miongoni mwa waliokamatwa kutokana na jaribio hilo.

Kwenye kikao na wanahabari jumatano jioni, mwendesha mashitaka wa Paris, Francua Molins amesema msako wa polisi kwenye kitongoji cha Saint Denis mjini Paris umetibua juhudi za kundi jipya la kigaidi.

Molins anasema, ushahidi wote, silaha zao, mipango na matarajio yao vimeonesha kuwa watu hao walikuwa tayari kutekeleza operesheni za kigaidi.

Anasema watu wawili waliuwawa kwenye msako huo. Wachunguzi wanaendelea kujaribu kuwatambua ,lakini inakuwa vigumu kutokana na nguvu zilizotumika wakati wa operesheni hiyo. Nyumba waliokuwemo washukiwa iliharibiwa vibaya na pia mmoja wao anaeaminika kuwa mwanamke alijilipua wakati wa operesheni hiyo.
www.voaswahili.com

NO COMMENTS