Lissu Agomea Mahakamani Akihofia Kukamatwa

0
222

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Mawakili nchini (TLS), Tundu Lissu mapema leo amegoma kutoka ndani ya mahakama ya Dodoma akihofia kukamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.
 
Lissu ambaye alifika mahakamani hapo kwa ajili kuwatetea wateja wake, inadaiwa kuwa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kumkamata, jambo ambalo alilibaini na kukatalia ndani ya mahakama hiyo.
 
“Waje wamkamate Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika ndani ya mahakama aliyokuwa akifanya kazi. Tatizo kubwa ni kwamba tunakamatwa kwa kutekeleza wajibu wetu wa kutoa maoni kama raia wa Tanzania,” alisema Lissu.
 
Aidha haijafahamika ni kosa gani ambalo polisi wanataka kumkamata Lissu.
UPDATES:
Lissu ameachiwa aondoke baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kufika mahakamani hapo na kueleza kuwa hajatoa maagizo kwa polisi yeyote kumkata mbunge huyo.
SOURCE:Globalpublishers.com

NO COMMENTS