Lebron abadili dini

0
515
Miamba ya Miami Chris Bosh,Dwayne Wade na Lebron James
Miamba ya Miami Chris Bosh,Dwayne Wade na Lebron James

Baada ya Lebron James kuondoka Cleveland nini kinachofuata washabiki wa Cleveland wameudhika vibaya sana mpaka kuchoma jezi yake  na mengi mengine, sasa je swali ni kuwa hakuna masiha baada ya Lebron na je huo ndio  mwanzo wa mwisho wa Cleveland Cavaliers?  Na je Cleveland hawataweza kufurukuta tena?

Mchambuzi mmoja wa michezo alisema habari njema kwa Cleveland ni kwamba timu zote zilizowahi kuchukua ubingwa zimewahi kufanya hivyo bila Lebron James. Na kwa maana hiyo kama Cleveland wakijitutumua na kuwabakisha wachezaji wao na pengine kupata wengine wazuri wataweza kufanya maajabu. 

Lakini hasira ya nini mashabiki wa Cleveland Lebron amekaa timu hiyo kwa miaka 7 mpaka alipotangaza kuondoka je kuna ubaya gani? matamshi aliyotoa mmiliki wa klabu hiyo ya Cleveland Cavaliers Dan Gilbert  yalikuwa ni ya kusikitisha na makali mno  ambapo mpaka ilibidi apigwe faini na shirikisho la mpira wa kikapu mpaka mtetezi wa haki za kiraia Jesse James aliingilia kati na kumsema kuwa anamwona kama Lebron ni mtumwa wake ambaye hastahili kuondoka?! kwani huu ulitakiwa kuwa ni uhusiano wa kibishara na Lebron alifanya kazi kwa muda wake wote mpaka mkataba wake ulipokwisha.

Hii imekuwa ni kama kubadili dini kwani Lebron alianza kuichezea timu ya Cleveland akiwa na umri wa miaka 17 baada tu ya shule ya sekondari.

Baada ya kuwa MVP kwa miaka miwili mfululizo na kuwa mchezaji wa kutegemewa na hatimaye amekuwa nguzo kuu ya timu hiyo ya Cleveland Cavaliers. 

Kuhama kwa Lebron kulikuwa gumzo kubwa hapa nchini wachambuzi mpaka yalichangiwa na Rais wa Markani Barack Obama akimtaka Lebron abaki Cleveland. Lakini Lebron amesema baada ya kujiuliza  kwa muda mrefu na kushauriana na mama yake ameamua kwenda Miami Heat ambapo ameungana na Chris Bosh na Dwayne Wade.

KILICHOMSUKUMA:

Lebron anataka pete yaani ubingwa na wachambuzi wanasema ameungana na marafiki wawili Chris Bosh na Dwayne Wade na  akijibu swali kuhusu historia ya NBA ambayo amekuwa akiisoma kwa muda ni Lebron alisema kwamba ligi hii unaweza kuwa staa mtu mmoja lakini kupata ubingwa unapata kama timu.

Kila la kheri Lebron kwenye timu yako mpya na jezi namba 6 ya Miami Heat ambayo inategemewa mwakani itatoa upinzani mkubwa kuchukua ubingwa wa kanda ya mashariki kutoka kwa mabingwa wa kanda hiyo Boston Celtics wakiwa na miamba mitatu.

NO COMMENTS