Laurent Gbagbo na mkewe wawekewa vikwazo

0
372


Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast aliyekataa matokeo ya kushindwa kiti cha urais nchini humo awekewa vikwazo.

Mke wa rais Laurent Gbagbo pia awekewa vikwazo.

Umoja wa Ulaya unasema rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Bagbo na mke wake ni miongoni mwa watu 19 ambao wamewekewa vikwazo kutokana na mzozo wa uongozi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) msemaji wa Umoja wa Ulaya aliwaambia waandishi wa habari huko Brussells Jumatatu kwamba jumuiya hiyo yenye wanachama 27 itapitisha vikwazo rasmi baadaye wiki hii.

Vikwazo hivyo vinategemewa kuwa ni pamoja na kuzuia mali zao na kutowapa viza Bw. Gbagbo na mkewe Simone na maafisa wengine 17.

NO COMMENTS