Lady Jaydee na Atemi watoa kibao kipya.

0
359

150403102103_atemi_640x360_bbc_nocredit
Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina ‘MOYO’.

‘Moyo’ ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .

Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.

Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni ‘single’ ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.

Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi ‘Usijali’ akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.
BBCSWAHILI

NO COMMENTS