LADY GAGA ATOA MPYA

0
397
Lady Gaga
Lady Gaga

Mwanamuziki mwenye machachari mengi Lady Gaga kama kawaida yake kila siku hutoa staili mpya ya nywele au mavazi safari hii kwenye tuzo za video bora za mwaka 2009 alifanikiwa kupata tuzo 8. Na si hivyo tu aliingia na staili ya aina yake ya nguo ambayo imetengenezwa kwa  nyama ya ng’ombe. Lakini wale waliokaa karibu naye wamesema nyama hiyo ilikuwa  haitoi harufu yeyote. Haya yetu macho sijui safari ijayo atakuja na nini.  Nguo hiyo imetengenezwa na designer Franc Fernandes na alipoulizwa na MTV alisema huko kwao Argentina inaitwa Matambre. Wamesema nguo hiyo hivi sasa imehafidhiwa kwenye makumbusho ya nguo zake. Na sasa yuko kwenye maandalizi ya kutoa  albam yake mpya  iitwayo “Born This Way” ambayo aliitangaza kwenye usiku huo  aliopokea tuzo hizo.

NO COMMENTS