KWAYA YA VIJANA KKKT IRINGA NA MWIMBAJI MWASONGWE KUFUNIKA TAMASHA YA UIMBAJI MAFINGA, KIPANGULA KUWA MGENI RASMI

0
487
Image result for ambwene Mwasongwe
Mwimbaji Ambwene  Mwasongwe
WAKATI
siku  za tamasha  kubwa la  kihistoria mjini Mafinga  mkoani Iringa
zimezidi  kusogea  ,mkuu  wa   jimbo la kanisa la  Kiinjili la Kilutheri
Tanzania  (KKKT) jimbo la Mafinga  mchungaji Antony Kipangula ndie
atakayezindua tamasha   hilo .
Image result for Kwaya  ya vijana KKKT Iringa
Kwaya  ya  vijana KKKT usharika wa Iringa mjini siku ilipotembelea  bungeni Dodoma
Akizungumza leo  na mwandishi wa habari hizi ,Mratibu  wa  tamasha   hilo Mary 
Mungai  aliyesa   kuwa uzinduzi  wa  tamasha  hilo utakwenda  sambamba
na uzinduzi  wa  ukumbi wa  kisasa KWA  AJILI ya burudani na shughuli
mbali mbali  ukumbi wa MAM ulipo katikati ya mji wa Mafinga  na  kuwa 
washindi  wa uimbaji KKKT nchini  kwaya ya vijana   usharika  wa kanisa 
kuu Iringa na mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu nchini Ambwene
Mwasongwe  wataongoza kupamba tamasha  hilo pamoja na kwaya  nyingine
na  waimbaji binafsi kutoka  ndani na nje ya Mafinga .
”  kutakuwa na  waimbaji  wengine mbali mbali pamoja na
burudani nyingine na  kuwa  lengo  la tamasha  hilo  pamoja na kutoa 
burudani kwa  wakazi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Iringa  na Njombe 
bado itakuwa ni  siku ya  uzinduzi
wa   ukumbi wa  burudani na sherehe mbali mbali katika mji huo wa Mafinga”
Mungai
alisema  kuwa  kwa ajili ya  kuwashukuru  wananchi wa mji  wa Mafinga 
kwa
ushirikiano mbali mbali ambao  wameendelea  kuutoa amelazimika  kuandaa
tamasha hilo ambalo  wananchi  watashuhudia  kwa  kiingilio kidogo 
sana  kama  sehemu ya kuchangia  gharama ndogo ndogo  za  maandalizi ya 
tamasha  na mchango kwa  V.I.P  utakuwa ni Tsh 10,000  wakati kawaida
kwa  watu  wazima ni Tsh 5000 na watoto ni Tsh 3000 pekee  na  kuwa 
ili  kuepusha  msongamano mlangoni tiketi  tayari zinauzwa katika  ofisi
ya  shule ya Southern Highlands Mafinga , Hazina Bima na 
Stationary ya Huruma Msigala na getini pia  zitauzwa .
Alisema  
pamoja na  kuwa  wilaya ya  Mufindi  ni moja kati ya  wilaya  zenye 
uchumi  mkubwa  hapa nchini na  watu  wake  ni  wale  wanaopenda
burudani  mbali  mbali  zikiwemo  za matamasha ya  nyimbo  za  injili 
ila bado kumbi nyingi zilizokuwepo haziwezi  kukidhi mahitaji ya
burudani  na kuwa  kuzinduliwa  kwa  ukumbi huo  kutafungua  milango ya 
uchumi kwa  mji   huo kwa    wadau kutoka ndani ya wilaya ya  Mufindi
na nje ya  mkoa kufika  kuutumia ukumbi huo kuandaa burudani mbali mbali
na hata  kuutumia kwa mikutano mikubwa . 
Mwenyekiti
wa  kwaya  ya  vijana usharika wa kanisa  kuu Kombo Mdegella
akizungumzia juu ya maandalizi ya ushiriki  wao katika  tamasha  hilo 
alisema  kwaya yake  ambayo  imekuwa  ikifanya  vema  katika mashindano
mbali mbali ya  uimbaji ipo  kwenye maandalizi makubwa ya  kuhakikisha
wanatoa burudani ya nyimbo  kali  kwenye Tamasha   hilo .

 ukumbi pekee katika mikoa ya
nyanda za  juu kusini kujengwa  kisasa na utakuwa na majukwaa mawili 
moja la kati  litakuwa ni  jukwaa  linalotembea pia  kutakuwa na V.I.P
kwa wageni maalum ambao ili  waweze  kuingia ukumbini watapandishwa
ghorofani  kwa ngazi maalum   na  kushuka kwa  ngazi hadi 
jukwaani iwapo watataka  kutoingilia mlango wa waalikwa  wote .

NO COMMENTS