Kutana na washiriki wa Growing up African

0
442

Mama Vicky

Ma Vicky huyu ndiye mama mzazi wa washiriki wa show hii alikuja na watoto wake wakiwa wadogo kabisa hapa Marekani. Alikuwa akifanya shughuli zake Tanzania akaamua kuja Marekani na wanawe na yeye ndio Baba na mama katika familia hapa Marekani kwani mzazi mwenzake anaishi Tanzania.
Eliza Lujwangana

Wa pili kushoto ndiye dada mkubwa Eliza Lujwangana ambaye kwa kiasi kikubwa anawasimamia wadogo zake na kuwapa mwelekeo anawajali mno wadogo zake kiasi kwamba hufikia kujisahau kwa ajili yao.
Bea

Huyu ndiye Bea yeye hupenda masuala ya fashen na urembo na haogopi kujituma ni mfano mzuri kwa ndugu zake.
Jessica

Jessica yeye ni kama mwajibikaji mkuu wa familia, msimamizi mzuri wa matumizi ya fedha na siku zote huhakikisha mama yao yuko salama.
Johnson Boy

Huyu ndiye Johnson Boy kama wanavyomwita kijana mwenye bidii sana ya kazi, mawazo ya kibiashara bna kuna jambo lolote la kufanya yuko tayari wakati wowote na yuko tayari kufanya lolote mradi la mafanikio mema na bora.
Andrew Felix

Andrew Felix ndiye mdogo katika familia kwasababu ndiye kitinda mimba utafikiri anafanyiwa kila kitu kwenye familia lakini la hasha ana mengi yanayoendelea ukimjua kwa undani atakushangaza.
Walipowasili Marekani

Familia ya Lujwangana walipowasili Marekani kwa mara ya kwanza.

NO COMMENTS