KUMI BORA YA BILLBOARD

0
523


Rihana anatamba na nyimbo mbili zikishika nafasi ya 7 na ya 2 kwenye chati za Billboard.

Kumi bora kwa mujibu wa jarida la Billboard wiki hii ni kama ifuatavyo katika nambari 10 wapo kundi la Black Eyed Peas na wimbo “The time” (Dirty bit) wakati Katy Perry amekamata nambari 9 na wimbo wake Firework kutoka kwenye albam yake Teenage Dream. Mwanadada huyu mwenye umri mdogo sana ameshatoa single 7 ambazo katika hizo 6 zimeshaingia kwenye kumi bora.

Namba nane ni kundi la Glee na wimbo wao stuck Like Glue na katika nambari saba kuna wimbo wa Rihana na Drake na wimbo What’s My name katika nambari sita yupo Kesha na wimbo wake “We are who we are” wakati namba tano ni mwimbaji mkongwe Nelly na wimbo “Just a Dream” kutoka albam yake Nelly 5.0 akiwa ameuza albam milioni 27 anashikilia nafasi ya mwanamuziki wa tatu kuuza albam katika muongo uliopita nyuma ya Eminem na Usher.

Kutokana na kutokuwepo kwenye orodha ya BET ya marapper 10 bora wa karne ya 21 amesikitika akisema hajapewa heshima yake anayostahili Nelly amesikitika sana.


Katy Perry anakamata nambari 9

Mwanamuziki mwenye mbwembwe Pink amekamata nafasi ya nne na wimbo wake “Raise your Glass” na hivi sasa mwanadada huyu anatarajia mtoto wake wa kwanza. Wakati huo huo Bruno Mars na wimbo wake “Just the way you are” ndiye anayeshikilia nafasi ya tatu mwanamuziki huyu ana kesi hivi sasa ya madawa ya kulevya ambayo inategemewa kusikilizwa Desemba mwaka huu.

Mwanamuziki mashuhuri kijana Rihana ameingiza wimbo mwingine tena katika kumi bora ukiwa unashika nafasi ya pili wimbo “Only girl in the world” kutoka albam yake “LOUD”. Mwanadadad huyu alifungua pazia katika tuzo za muziki wa Marekani (AMA) Jumapili iliyopita na pia kupata tuzo ya mwanamuziki bora wa kike.

Na katika nambari moja lipo kundi la Far East Movement wakishirikiana na Cataracs na Development na wimbo “Like a G6”.

Kundi lililoshika nambari moja kwenye chati za Billboard Fareastmovement.

NO COMMENTS