Korea kaskazini hatari ya vita inanukia

0
1765

Rais Barack Obama na rais wa Korea Kusini Lee Myung-bak
Huko Korea hali imeendelea kuwa tete na leo hii milio mipya ya mizinga inatishia rasi ya Peninsula na kupelekea mfuatano wa maonyo mapya wakati mvutano ukiongezeka kati ya kaskazini na kusini.

Kwa mujibu wa Sauti ya Amerika wakazi katika kisiwa cha Korea kusini cha Yeonpyong waliripoti kusikia milio ya makombora kutoka Korea kaskazini lakini maafisa wa kijeshi wa Korea Kusini wamesema hakuna makombora yaliorushwa kwenye eneo lao lakini tukio hilo limekuja siku tatu tu baada ya mashambulizi ya makombora ya Korea kaskazini kwenye kisiwa hicho na kuuwa wanajeshi wawili na raia wawili na kujeruhi wengine 18.

Hali hii inaelekea kuleta hatari ya kuanguka vita alisema Peter Beck mtafiti katika taasisi ya baraza la sera za mambo ya nje ya Marekani alipohojiwa na jarida la Express mjini Washington Dc.

Rais wa Korea Kusini amesema baada ya lile shambulizi la kwanza kwamba Korea Kusini haitaweza kuvumilia mashambulizi kama hayo kwa raia wake.

Naye rais wa Marekani Brack Obama alielezwa kukasirishwa sana na kitendo hicho cha Korea Kaskazini na kusema kwamba Marekani itaendelea kuilinda na kuinga mkono Korea Kusini na si hivyo tu ametuma meli ya kivita iliyo na uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.
Mlolongo wa historia ya mgogoro wa nchi hizi ni kama Ifuatavyo:
Juni 25,1950 :Korea kaskazini yaivamia Kusini na kupelekea vita vya Korea.
July 27,1953 :Vita vya Korea vyamalizika
January 1968:Makomando wa Korea Kaskazini wavamia nyumba ya Rais wa Kusini (Blue House) na kuuwa askari 7 wa Korea Kusini katika jaribio la kumuuwa rais Park Chung Hee lililoshindwa.
August 1974:Mke wa rais Park auwawa katika jaribio la kumuuwa rais huyo.
Oktoba 1983:Rais wa Korea Kusini Chan Doo-hwan aepuka jaribio la kuuwawa kwa bomu huko Myanmar.
Novemba 1987:Abiria 115 wauwawa baada ya ndege ya Korea Kusini kulipuliwa na ambapo majasusi wawili wa Korea Kaskazini wakutwa walihusika.
Juni 1999: Wanajeshi 7v wa Korea Kusini wajeruhiwa na wengine 20 hadi 30 wa Kaskazini wauwawa baada ya wanajeshi Kaskazininkukatiza mpaka wa Yellow Sea kwa zaidi ya siku 9.
Novemba 2009:Korea Kusini yadai imeuwa mwanajeshi mmoja wa Kaskazini baada ya pande hizo kushambuliana katika mpaka wa Yellow Sea.
Machi 2010:Bomu lazamisha manowari ya Korea Kusini na kuuwa wanajeshi 46 baada ya uchunguzi yagundulika Korea Kaskazini walihusika.

NO COMMENTS