Kiongozi wa Democratic nchini Marekani kujiuzulu

0
333

Kiongozi wa Chama cha Democratic nchini Marekani amesema atajiuzulu baada ya barua pepe zilizofichuliwa na kuchapishwa na mtandao wa WikiLeaks kudokeza huenda maafisa wakuu wa chama walijaribu kuvuruga kampeni ya Bernie Sanders.

Ufichuzi huo umetishia kuvuruga umoja katika chama hicho.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders, alikuwa amemshinikiza Debbie Wasserman Schultz, mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama cha Democratic, ajiuzulu mkesha wa kufanyika kwa kongamano.

Bi Hillary Clinton, aliyekuwa akishindana na Bw Sanders katika kutafuta tiketi ya chama cha Democratic, anatarajiwa kuidhinishwa rasmi kuwa mgombea katika kongamano kuu la chama mji wa Philadelphia.

Bw Sanders alisema Bi Wasserman Schultz “hafai kuwa mwenyekiti” wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama cha Democratic.

“Na nafikiri barua pepe hizi zinatilia mkazo msimamo wetu kwamba hafai kuwa mwenyekiti,” ameambia kipindi cha This Week cha runinga ya ABC.

Kwa muda mrefu kambi ya Bw Sanders imekuwa ikimtuhumu Bi Wassermann Schultz na wakuu wengine wa chama kwa kumpendelea Bi Clinton.

Chanzo: BBC Swahili160725053622_debbie_wasserman_schultz_640x360_reuters

NO COMMENTS