Kila la kheri Taifa Stars

0
1004

Taifa Stars

Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” jumamosi inajitupa uwanjani huko Daresalaam Tanzania katika michuano ya kuwania tiketi ya kushiriki katika kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Morrocco mwaka 2012. Katika mchuano huo kabambe wa kundi D Stars wanahitaji ushindi na kutumia nafasi ya uwanja wa nyumbani kuwaangusha hao vigogo wa soka Afrika timu ya Morocco. Stars ilianza vizuri kampeni yake baada ya kutoka sare na Algeria huko Algiers katika mchezo wake wa kwanza na sasa wana kazi nyingine lakini mchezo wa kwanza umewapa moyo kuwa wanaweza.

Timu ya Morocco imeshaita wachezaji wake wa kulipwa ikiwa ni pamoja na mshambuliaji hatari Morouane Chamakh wa Arsenal ya Uingereza. Nao Taifa Stars pia imeita vijana wake wanaocheza soka ya kulipwa nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Dan Mrwanda anayecheza Vietnam na Henry Joseph anayecheza Norway.

NO COMMENTS