Kheri ya “Thanksgiving” au siku ya Bata

0
739
Nyama ya bata iliyotengenezwa kwa umahiri.

Hivi sasa hapa Marekani wananchi wanajiandaa na sherehe za Thanksgiving au sherehe za shukrani ambazo si za kidini lakini ni sherehe ambazo huadhimishwa Marekani na Canada. Kihistoria  zilikuwa ni sherehe za kutoa shukrani kwa mavuno ya mwaka . Lakini sherehe hizi huadhimishwa pia Uholanzi .

Hivi sasa inaadhimishwa kwa watu kupika vyakula kede  kede na hasa Bata Mzinga lazima awepo kwenye mlo wa siku, na hivyo basi makampuni mbali mbali  pia hutoa zawadi ya bata mzinga kwa wafanyakazi wao  katika kipindi hiki.

Si hivyo tu katika majumba mbali mbali na maofisi  Bata mzinga lazima awepo kwenye maakuli na hivyo basi siku hii pia hujulikana kama siku ya Bata. Na siku hii ilitangazwa kwa mara ya kwanza na Rais Abraham Lincoln kuwa sikukuu ya kitaifa mwaka 1941 baada ya kupitishwa na bunge la Marekani.

Siku hii ni inaadhimishwa Alhamisi ya mwisho ya mwezi Novemba kila mwaka hapa Marekani na katika siku hii Bata Mzinga milioni 45 wanachinjwa na kuliwa Marekani na si hivyo tu mtu mmoja anakadiriwa kula kiasi cha kalori 4500 kwa siku moja! Ama kwa hakika ulaji unakuwa si wa kawaidana pia ni wakati wa wafanya biashara kuvuna fedha maana maduka yote ndio tyanaanza kuuza vitu kwa bei maalum ya punguzo kuanzia Alhamisi saa 10 Alfajiri na kuendelea wakati maduka yanabaki wazi usiku kucha.

Kwheshima na taadhima kwa niaba ya blog hii nawatakia wote Kheri ya siku ya Bata  na msile sana mkavimbiwa matumbo maana vyakula ni vingi vinatia kishawishi kikubwa lakini waswahili husema  raha  jipe mwenyewe na nyama Bata itamu.

NO COMMENTS