Katibu mkuu wa CCM ahani msiba wa hayati mzee Luangisa mjini Bukoba.

0
778
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni  mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa
mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu
cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa
nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA.

NO COMMENTS