Kara DioGuardi aweka manyanga chini Amerikan idol kulikoni?

0
416
KaraDioGuardi jaji wa zamani wa Amerikan idol
KaraDioGuardi jaji wa zamani wa Amerikan idol

Jaji wa Amerikan idol Kara Dio Guardi ambaye ni shoga wa karibu wa jaji mwingine wa zamani Paula Abdul ambaye inasemekana ndio aliomleta kwenye show hiyo ameamua kufuata nyayo za rafiki yake.

Kwa mujibu wa Access Hollywood jaji huyo msanii, mwandishi wa nyimbo na Afisa wa juu wa kampuni ya kurekodi miziki ya Warner bros ameamua kutangaza kujiuzulu kwake Ijumaa . Taarifa hii ya Kara imekuja kwa mshangao kwani ni miezi miwwili tu iliyopita alipotangaza kuwa yuko tayari na akisubiri kwa hamu ujio wa  msimu ujao wa 10 wa mashindano hayo ambao utakuwa bila jaji mwenye utata mkubwa Simon Cowell.

Huyu atakuwa ni jaji wa atu kuacha show hiyo kufuata nyayo za jaji mwanzilishi Paula Abdul halafu Ellen Degenrous aliyechukua nafasi ya Paula na Simon Cowell ambao wote walitangaza kuondoka kwa nyakati tofauti.

Hivi sasa jajimwanzilishi wa show hiyo  aliyebaki ni Randy peke yake na tayari kuna majina ya watu maarufu mbali mbali waliotajwa kuingia kwenye show hiyo ikiwa ni pamoja na Jenniffer Lopez na Steve Tyler wa Aerosmith.

Inaonekana kuna malumbano kati ya majaji na halikadhalika mambo ya fedha kwa maana Paula Abdul alitaka kuongezwa fedha lakini ikashindikana na vile vile kulizuka uvumi kuwa haelewani na jaji mwenzake  Simon Cowell na pia alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa washindani na hatimaye  akaamua kuondoka .

Je ni nini kilichomsibu Kara?au Fox wameamua kumuondoa kwenye show kuna uvumi kuwa huenda Fox wameamua kufanya hivyo  lakini Fox hawajathibitisha habari hiyo lakini kwa ujumla show  hii itachukua sura mpya kabisa kuanzia sasa kwenda mbele na haijulikani kama itaendelea kuwa na umaarufu kama ilivyokuwa hapo awali au itakwenda chini.

NO COMMENTS