KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA LINAKUKARIBISHA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA OYES 2016.

0
452

KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LILILOPO SASABASA ILELEMA JIJINI MWANZA
CHINI YA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA, LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA MKUTANO
MKUBWA WA INJILI UITWAO “OPEN YOUR EYES AND SEE” KWA KIFUPI “OYES CONFERENCE” UKIWA
NA MAANA “FUNGUA MACHO NA UONE” AMBAO HUFANYIKA MARA MOJA TU KWA MWAKA.
MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA EAGT LUMALA
MPYA KUANZIA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 12 MWEZI WA 6 HADI TAREHE 19 MWEZI WA 6
MWAKA HUU, KUANZIA SAA 8 KAMILI MCHANA HADI SAA 12 ZA JIONI.
KATIKA MKUTANO HUO, MHUBIRI WA KIMATAIFA KUTOKA OTTAWA NCHINI
CANADA ALIEKUFA NA KUFUFUKA BAADA YA SIKU NNE, MAMA DOMITILA NABIBONE, PAMOJA
NA MCHUNGAJI JARED MLOGECHA KUTOKA BOSTON MASACHUSSETS NCHINI MAREKANI, WATAKUWEPO.
WAIMBAJI MBALIMBALI AKIWEMO MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA JIJINI DAR
ES SALAAM, CHAMWENYEWE JEMBE KUTOKA MOROGORO, NA KUTOKA MWANZA HAVILLA KWAYA,
HOT SPEARS KWAYA, AGNES AKRAMA,THEO DAV, HAPPY SHAMAWELE, JOSEPH RWIZA,
MITAGATO, SARAH GAGALA PAMOJA NA CHACHA WATAHUDUMU KATIKA MKUTANO HUO.
ILI KUFIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA, PANDA MAGARI YA AIRPORT AU
ILEMELA, SHUKA KITUO CHA SABASABA KONA YA KISEKE, TEMBEA HATUA CHACHE HADI SOKO
JIPYA LA SABASABA, ULIZA KANISA LA MCHUNGAJI DR.DANIEL MOSES KULOLA UTAELEKEZWA.
USIKOSE KUFUATILIA MAHUBIRI YA MKUTANO HUO KATIKA RUNINGA YAKO
PENDWA YA STAR TV KUPITIA KING’AMUZI JABARI LA VING’AMUZI CHA CONTINENTAL
PAMOJA NA 96.8 AFYA RADIO.
WALETE WAGONJWA NA WENYE MAHITAJI MBALIMBALI ILI WAFUNGULIWE KWA
JINA LA YESU. KWA USHAURI NA MSAADA WA KIROHO, WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU, MCHUNGAJI
DR.DANIEL MOSES KULOLA, KWA NAMBARI ZA SIMU 0767 74 90 40 AU 0784 74 90 40
Bonyeza Hapa Kusikiliza Au Play Hapo Chini.

NO COMMENTS