Justin Bieber ashinda msanii wa mwaka

0
1661

Justin Bieber akifanya vitu vyake.
Justin Bieber ndiye mwanamuziki bora wa mwaka wa Marekani alitangazwa katika tuzo za wanamuziki wa Amerika baada ya kutoka na tuzo nne kwa ujumla ikiwa ameweka historia ya kuwa mwanamuziki mdogo kuliko wote kushinda tuzo ya mwanamuziki bora wa mwaka Marekani.

Alikuwa ni nyota wa usiku huo wa Jumapili lakini kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ni kwasababu ya kuruhusu za kura za mtandao ambazo kwa kiasi kikubwa watoto wengi wanaompenda mtoto huyo mwenzao wanaweza kupiga kura.

Na katika hotuba yake aliwashukuru Michael Jackson na Usher Raymond kwa kuwa watu muhimu sana katika maisha yake waliomsaidia sana na hatimaye kumwita Usher Raymond mbele wakati akipokea tuzo yake na kumkumbatia kwa shukrani ya kuwa mwalimu katika maisha yake.

Justin mwenye umri wa miaka 16 tu aliyekulia huko Ontario Canada aligunduliwa kwenye mashindano ya vipaji alipokuwa na miaka 12 tu ambapo alishika nafasi ya pili.

NO COMMENTS