JOZI LOUNGE YADHAMINI MISS TANZANIA 2016

0
663
Club maarufu
kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jijini Dar Es Salaam, imejitokeza hivi
karibuni kujiunga na moja katika kampuni na taasisi zilizokwisha kujitokeza
kudhamini zoezi zima la kutafuta mrembo wa tanzania atakayepeperusha na
kuitangaza Tanzania katika anga za kimataifa katika Nyanja mbalimbali yakiwemo
utalii na huduma ya jamii yenye mahitaji maalum.

Akizungumza
na warembo kutoka mikoa yote Tanzania ambao wanatarajia kuchuana vikali
mwishoni mwa mwezi wa kumi huko jijini Mwanza na hatimaye kumpata mshindi wa
Miss Tanzania 2016, Mkurugenzi wa Jozi Lounge Bw.Dismas Massawe amesema Jozi
Lounge itawadhamini warembo hao kwa kuwapatia malazi, chakula na mahitaji
mengine muhimu kwa kipindi cha siku tatu ambapo jana ilikuwa uzinduzi na leo ni
siku ya semina mbalimbali na siku ya jumapili itakuwa siku ya kusherehekea
ushindi wa mikoa tayari kuelekea katika mapambano ya ngazi ya Taifa.

Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika moja ya pozi jana mara
baada ya kuwasili Jozi Lounge, ambapo watakuwa hapo kwa siku tatu
mfululizo. Jozi lounge ni mojawapo wa wadhamini wa mashindano ya miss
tanzania mwaka huu 2016
 Wakipata vinywaji kwa pamoja huku wakifurahia utulivu mwanana ndani ya Jozi Club
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2016,ambapo jana wameingia kambini pia walipata muda wa kuserebuka ndani ya Club maarufu
kwa jina la Jozi Lounge iliopo msasani jiji Dar EsSalaam.
 Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiserubuka ndani ya Jozi Club kwa raha zao

NO COMMENTS