Je Dr Slaa ni tishio kwa CCM?

0
556
Mgombea wa Chadema Dr.Wilbroad  Slaa
Mgombea wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa

Chama tawala nchini Tanzania cha CCM kimeonekana au kuonyesha kumzungumzia mgombea urais wa upinzani na katibu mkuu wa chama cha Chadema Dr.Wilbroad Slaa. Hii imetokana na mgombea wa chama tawala Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  J.K kutoa onyo kwa chama hicho kutobweteka na kuwa macho na wapinzani akimtaja Dr.Slaa.

Wachambuzi wa siasa za Tanzania wanachojiuliza ni kwamba mbona wagombea wengine hawakutajwa isipokuwa Dr.Slaa? mgombea huyu wa urais kupitia Chadema alikuwa mmoja wa wabunge machachari waliotoa hoja nzito sana bungeni na zilizowapa taabu viongozi wa chama tawala ikiwa ni pamoja na orodha ya mafisadi.

Mgombea huyu ambaye alikuwa ni mbunge wa Karatu kwa kupitia Chadema yeye na chama chake wameomba mdahalo na wagombea wengine wa urais lakini chama tawala kupitia katibu mkuu wake Bw.Yussuf Makamba  kimeeleza kutokuwa tayari kwa mgombea wao rais wa jamhuri ya muungano kushiriki, Chadema tayari wameshatoa maelezo kwamba katibu mkuu wa chama tawal Yussuf Mkamba anaogopa mgombea wake rais wa jamhuri ya muungano kupambana nao kwenye mdahalo kwani tayari Dr.Slaa akiwa na orodha ya mafisadi 11  atadai majibu kwa rais ambayo inaweza ikawa ngumu kwa rais kujibu.

Katika karne hii ya 21 kampeni za uongozi za kila nchi iliyoendelea zinakwenda sambamba na midahalo ya wagombea kwani hiyo inawapa wananchi nafasi ya kufahamu zaidi wagombea wao wana sera gani na si hivyo tu wakati wa 2005 nchini Tanzania mdahalo ulifanyika kati ya wagombea urais wa wakati huo.

Je lipi ni la ajabu leo  hii kwamba chama tawala hakitaki kufanya mdahalo? Rais Kikwete amekuwa akitumia vyombo vya habari na mtandao pale alipofanya mahojiano na wananchi kupitia TvT na kuonyesha kuwa Rais mwenye nia ya kuwa wazi mbele ya wananchi wake sasa leo imekuwaje?  mpaka chama chake kinakataa kufanya mdahalo?

Chadema wakisema kwamba kuna mambo wanayoficha je watapinga na kwa hoja gani? sikuzote mdahalo unawapa wananchi nafasi ya kujionea wagombea wakishindana kwa nguvu za  hoja na  katibu mkuu wa CCM huu ni wakati wa kuwa wazi na kufanya mdahalo ili wananchi wapate nafasi ya kuwasikia viongozi wao wakishindana kwa hoja, tatizo liko wapi mbona Mkapa alikubali kufanya mdahalo 1995?

Chama cha  ccm na Chadema vimeshutumiwa kufanya kampeni mapema kabla ya wakati wake na baadhi ya vyama vya upinzani vikimtaka msajili wa vyama John Tendwa achukue hatua. Kampeni zinatakiwa kuanza rasmi Agosti 20 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi wa Tanzania. Katika kile walichodai ni kuomba udhamini kwa wananchi wagombea hawa wa CCM na Chadema wamekuwa wakipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi kitu ambacho wenzao wamedai ni kampeni za mapema kwa hiyo waonywe au kuenguliwa kugombea lakini hilo linawezekana kweli?

Dr Slaa akiwasilimia wafuasi wake kwenye moja ya mikutano
Dr Slaa akiwasilimia wafuasi wake kwenye moja ya mikutano

NO COMMENTS