Ivory yasimamishwa uanachama AU-Lamamra

0
396

Rais Laurent Gbagbo aliyekataa matokeo ya kushindwa akiwa na baraza lake la mawaziri.

Umoja wa Afrika imesitisha uanachama wa Ivory Coast, kwa sababu rais Laurent Gbagbo amekataa kukabidhi madaraka baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika (VOA) kamishna wa ulinzi na amani wa Umoja wa Afrika, Ramtane Lamamra, alisema Alhamisi kwamba Ivory Coast imesimamishwa kushiriki shughuli zote za Umoja wa Afrika hadi rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Alassane Ouattara, akabidhiwe madaraka.

Tume ya uchaguzi nchini Ivory Coast, ilimtaja bwana Ouattara mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita, matamshi yaliyoungwa mkono na Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa.
Kwa habari zaidi ungana na www.voaswahili.com

NO COMMENTS