Ivory Coast hali bado tete marais wawili waapishwa!

0
394

Kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara aliyetangazwa mshindi hapo awali na tume ya uchaguzi.
Maandamano ya mitaani yaliendelea leo katika mji mkuu wa boiashara wa Ivory Coast wakati kiongozi wa upinzani katika uchaguzi wa hivi karibuni wa rais akizidi kusisitiza kuwa ameshinda na ana haki ya kutawala.

Waunga mkono wa Alassane Ouattara ambaye alitangazwa mshindi wa kura ya duru ya pili ya Novemba 18 na tume ya uchaguzi ya Ivory Coast walionekana wakichoma magurudumu ya magari huko Abidjan.

Baraza la katiba la Ivory Coast limeunga mkono madai ya mpinzani wa rais aliyeko madarakani Laurent Gbagbo ambaye amesema alichaguliwa tena katika kura ya Novemba.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki anafanya kazi kwa niaba ya umoja wa Afrika ili kupata suluhisho kwa ugomvi huo.

Wakati huo huo Jumapili Bw. Ouattara na Gbagbo walitangaza serikali zao zinazopingana na kuapishwa kama marais wa nchi hiyo.

Chanzo:www.voaswahili.com

NO COMMENTS