Ivory Coast bado hakieleweki.

0
387


Kiongozi aliyegoma kushindwa Laurent Gbagbo.

Kiongozi anayetambuliwa na umoja wa Afrika na jumuiya ya kimataifa kuwa mshindi wa kiti cha urais Alassane Ouattara.

Hali bado ni tete huko Ivory Coast na kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (VOA) Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema walinda amani wataendelea kubaki Ivory Coast licha ya wito wa rais aliyeko madarakani Laurent Gbagbo kuwataka waondoke.

Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesema mpango huo utakamilisha wajibu wake na kuendelea kuangalia ghasia zozote nchini humo.

Msemaji wa Bw. Bagbo alisema katika televisheni ya taifa Jumamosi kuwa walinda amani wa umoja wa mataifa wamekiuka wajibu wao na kutaka vikosi hivyo pamoja na vile vya Ufaransa viondoke nchini humo.

Je Ivory Coast inaelekea wapi ? Afrika tunaelekea wapi? nchi hii hivi sasa ina viongozi wawili mmoja anaongoza kutoka Ikulu na mwingine kutoka kwenye hoteli, halikadhalika wanajeshi wamegawanyika wanaomuunga mkono Gbagbo na pia wanaoumuunga mkono Outtara.

NO COMMENTS