IBADA YA KUAGA MWILI WA MZEE EDDIS MGAWE SILVER SPRING, MD.

0
1225
Jeneza lililobeba mwili wa mpendwa Mzee Eddis Mgawe likiwa mbele ya Kanisa la Bethel World Outreach Church Lililopo Silver Spring, Maryland ilikofanyika Ibada ya misa ya kumuaga Mzee Eddis Mgawe siku ya Alhamis April 2, 2015 na Watanzania DMV na wengine kutoka majimbo mengine kujumuika pamoja na familia wakiwemo wafanyakazi wa Voice Of America (VOA) wakiongozwa na mkuu wa kitengo hicho cha idhaa ya kiswahili Dr. Hamza Mwamoyo. Mtoto wa marehemu, Mary Mgawe ni mfanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA na wafanyakazi wenzake walimchangia fedha za rambirambi.
Familia ikiaga mwili wa mpendwa wao kulia ni aliyeinamia jeneza ni mtoto wa marehemu Mary Mgawe.
Familia ikiaga mwili wa mpendwa wao na wapili toka kushoto ni mke wa marehemu mama. Margaret Mgawe.
Familia ikiwa na hudhuni kubwa huku watoto wa marehemu wakimfariji mama yao.
Wanafamilia wakiwa kwenye huzuni kubwa baada ya kuanga mwili wa mpendwa wao.
Mtunza mahesabu kamati ya msiba Bi. Seche Malecela akiongea kwenye ibada ya misa na kuaga mwili wa mzee Eddis Mgawe iliyofyanika siku ya Alhamisi April 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Mchungaji Dr. Nicku akifanya akifungua Ibada ya misa na kumuaga mzee Eddis Mgawe kwa maombi.
Mchungaji Igogo akiongoza Ibada.
Tino Malinda akisoma wasifu wa marehemu na kutoa shukurani za familia.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akiongea machache na kusisitiza upendo na mshikamano kwenye Jumuiya zetu.

Kwa picha zaidi bofya HAPA

NO COMMENTS