Huyu ndio msanii wa kwanza Bongo anayefanya ‘All White Party’ Marekani

0
109

Tanzania imebarikiwa kuwa na wasanii wengi wenye vipaji vya muziki ambavyo vinawakilisha vizuri katika nchi mbalimbali.

Miongoni mwa wasanii ambao wanaonekana kuwakilisha vizuri ni Babbi ambaye yupo nchini Marekani.

Msanii huyo anatarajia kufanya tamasha la show yake mwenyewe iitwayo ‘Babbi All White Party’ Jumamosi hii ambapo atakuwa msanii wa kwanza wa Bongo Flava kufanya kitu kama hicho nchini humo.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Phoenix Arizona, ambapo pia atafanya uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Kikomando’. Tayari msanii huyo ameshaachia nyimbo takribani tatu tangu mwaka huu ulipoanza.
CHANZO:GPL

NO COMMENTS