HUKU ‘NDOA’ YAKE NA UWOYA IKITIKISA…DOGO JANJA, WAMAMA SIRI 4 ZAVUJA!

0
89

SIKU zinakwenda kwa kasi kwani ni ‘majuzi’ tu zilisambaa taarifa za dogo anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kuwa alifunga ndoa isiyokuwa na vithibitisho na staa mkubwa wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya. Nyuma ya tukio hilo lililotikisa vilivyo, kuna siri nzito ambazo zimefichuka juu ya Dogo Janja kupendwa na mastaa waliomzidi umri ‘majimama’, Ijumaa lilidokezwa.

SIRI YA KWANZA
“Ninavyojua hakuna ndoa pale, namjua vizuri Uwoya, kwanza amezaliwa mwaka 1988 hivyo anakaribia umri wa miaka 30 na Dogo Janja amezaliwa mwaka 1997 na ana umri wa miaka 20. “Unajua Kibongobongo, wanaume wengi wamewazidi umri wake zao.
Ishu ya wanawake kuwazidi umri wanaume imeibuka kwenye kizazi tulichonacho na ndiyo maana uhusiano haudumu kwa sababu utakuta ‘mjimama’ mtu mzima anakuwa na ‘mtoto’ au ‘kiserengeti boi’ ambaye bado ana mambo mengi ya ujana. “Hata hivyo, kuna watu wanaamini kuwa umri ni namba tu na mapenzi ya kweli hayajali umri.

Ninachojua Dogo Janja na Uwoya ni washkaji tu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Kinachofanyika kuna watu wameamua kucheza na akili za Wabongo wasiokuwa na uwezo wa kuhoji, lakini pale hakuna ndoa. Na kama kweli kuna ndoa ninyi (Global) waambieni Uwoya na Dogo Janja waoneshe cheti cha ndoa.
“Kibaya zaidi hii ishu imeshirikisha watu wengi wenye heshima zao kama akina Madee, lengo likiwa nikutengeneza kiki kwa sababu kiki za Dogo Janja zilianza muda mrefu tangu jamaa huyo alipodai kuwa anamzimikia Uwoya tangu akiwa mdogo alikuwa anammezea mate runingani. “Huo ndiyo ukweli kwa sababu wakati Uwoya akiwa tayari ni staa miaka kumi iliyopita, Dogo Janja bado alikuwa shule ya msingi.”

SIRI YA PILI
“Kwa hiyo, watu wa karibu wote hadi wazazi wanajua tu ni kiki kwa sababu
Uwoya na Dogo Janja ni levo mbili tofauti kabisa kama mbingu na ardhi. “Tukiacha ishu ya Dogo Janja kutokuwa na mkwanja mrefu wa kumhudumia Uwoya pia maumbile yao yanapishana. Uwoya ile ni mashine kubwa wakati Dogo Janja ni kimbaumbau. Kama siyo kubemendwa huyo Dogo Janja anatafuta nini?
Ukitaka kujua kuna kitu huwa mastaa wenye umri mkubwa wanakitafuta kwa Dogo Janja, ndivyo ilivyokuwa alipohusishwa na video queen Agness Gerald ‘Masogange’aliyemzidi kwa umri wa miaka kumi kama ilivyokuwa kwa Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Muna Love na Feza Kessy ambao wote wamemzidi kwa zaidi ya miaka ishirini. “Siri ambayo wengi hawaijui ni kwamba, wanapohusishwa na Dogo Janja huwa kiki zao zinakuwa kubwa kwa sababu ya mijadala ambayo huwa inaibuka juu ya uhusiano huo hata kama ni wa kutengeneza.Kusoma zaidi bofya

SIRI YA TATU
“Ukiwaangalia mastaa hao anakuwa anahusishwa nao ni wale wenye makalio makubwa hivyo kutengeneza picha kwamba Dogo Janja ana ‘ugonjwa’ wa mijimama wenye ‘mizigo’ mikubwa. “Nilimsikia Dogo Janja siku moja akisema kuwa eti huwa ni kwake ni suna lakini pia huibua gumzo kubwa kwa kuwa yeye ni mdogodogo na wao ni ‘mizinga’ hivyo kila mtu hupenda kuwazungumzia.
SIRI YA NNE
Mbali na siri hizo tatu, pia kuna ishu ya kismati inaonekana kama anatumia ‘kamzizi’ katika kuwanasa. Unajua tangu yule dogo (Dogo Janja) anaingia kwenye sanaa, alionekana kabisa mwenye kismati cha kupendwa. Kwa hiyo inapotokea staa wa kike akahusishwa naye, basi huwa ni kiki kubwa kwa staa huyo kama ilivyotokea kwa Uwoya maana kila mtu anashangaa au kubisha kwamba haiwezekani wakawa wanandoa.” Lakini ukiachana na hayo yote, ameweka rekodi kwa wasanii wenzake wote wenye umri mdogo kufanya mambo hayo, amewapita Young Dee, Young Killer na wengineo.
IJUMAA MZIGONI
Kuhusu ishu hiyo, mara kadhaa Ijumaa lilizungumza na Uwoya ambaye aliishia kucheka na kudai kuwa ni filamu huku akihoji kama na yeye anafaa kuolewa? Kwa upande wake Dogo Janja aliliambia Ijumaa kwamba kwa sasa aulizwe juu ya ngoma zake na kazi zake za muziki na kuachana na ishu hiyo.
HABARI: GAZETI LA IJUMAA, NOVEMBER 2, 2017

NO COMMENTS