Hifadhi ya mlima Kilimanjaro yatangaza ofa kwa watalii wa ndani

0
341

iv class=”separator” style=”clear: both; text-align: center;”>

Mhifadhi utalii katka hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Eva Mallya akizungumza juu ya ofa
iliyotangazwa na hifadhi hiyo ya kupanda mlima huo kwa siku moja na
kurudi hadi kilele cha Shira.
Afisa masoko wa KINAPA
,Antypas Mgungusi akisistiza jambo wakati akizungumzia juu ya ofa ya
safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro huku akishauri wenye sherehe zao
kutumia nafasi hiyo kupanda Mlima huo kwa ajili ya kufanya sherehe
zao,alitaja sherehe ambazo zinaweza fanyika katika hifadhi hiyo ni
pamoja na wale wenye kukumbuka siku zao za kuzaliwa wanaweza fanya
hivyo wakiwa kileleni,lakini pia kwa wale wanaoenda Honey Moon baada
ya ndoa pia wameshauriwa kufanya hivyo katika kipindi hiki cha
ofa.
Baadhi ya watalii wa ndani
wakielekea katika kilele cha Shira safari ambayo inatajwa asilimia 70
wanaenda kwa usafiri wa gari 
Ukiwa katika hifadhi hiyo
utafurahia mandhari mbalimbali za mlima huo.
Wengine wanaweza pia kupanda
na watoto wao.
Hivi ndivyo safari ya mwisho
huwa.
Njiani utakutana na uoto
mbalimbali wa asili .
Zipo tenti kwa ajili ya
watalii wanaoendelea na safari.
Waliofanikiwa kufika kilele
cha Shira hawakusita kuonesha furaha zao kwa kucheza .

Na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya
Mlima Kilimanjaro 
(KINAPA)
imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani
ya 
kipindi cha miaka 10 huku
asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni 
wazawa.

Asilimia hiyo
inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda
Mlima 
huo kwa muda wa siku moja hali
inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo 
kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi
zetu ili kujionea 
urithi tuliopewa
na Mungu.


Mhifadhi utalii wa KINAPA,Eva Mallya alisema
katika kuhamasiosha 
utalii wa ndani
,KINAPA imeandaa zoezi maalumu ambalo litadumu kwa 
muda wa siku nne kwa watanzania walio walio karibu
na mlima kuweza

kuupanda kwa muda wa siku moja na
kurudi.


“Tumeandaa zoezi rahisi kwa kila mmoja mwenye
nafasi aweze 
kupanda,sehemu
kubwa itakuwa ni kwa kutumia gari ambapo walio
tayari 
watachukuliwa na gari hadi eneo
fulani kabla ya kutembea umbali mdogo 
na kutizama uwanda wa Shira katika mlima
Kilimanjaro.”alisema Mallya.


Alisema zoezi la
uandikishaji kwa ajili ya watakao penda kupanda 
katika mlima huo tayari limeanza katika vituo
vilivyoko jirani na Duka 
la Maua
mkabala na Rafiki Supermarket ,Hosptali ya rufaa ya KCMC
na 
njia Panda ya Himo.

Mallya alisema mpandaji atapaswa kujitegemea kwa
Sweta na Jacket kwa 
ajili ya baridi
,suruali raba pamoja na chakula huku mhusika
akitakiwa 
kulipia kiasi cha
sh 15,000 kama kiingilio cha hifadhini.


Kwa upande wake afisa masoko wa KINAPA,Antypas
Mgungusi alisema safari 
ya kupanda
mlima Kilimanjaro imekuwa ikitumiwa na baadi ya
watalii 
kufanya matukio ya kihistoria
ikiwemo kufunga ndoa na wengine

kuadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwa
kileleni.


“Imezoeleka kuwa watu wanapokuwa na matukio yao
yakiwemo ya 
mikutano,au Honey
moon baada ya ndoa na siku za kuzaliwa wamekuwa 
wakifanya sherehe zao mijini,lakini kuna maeneo
mengine kama haya ya

hifadhi kufanyia mambo hayo”alisema
Mgungusi.


Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu
duniani kwa kuhifadhi 
barafu kwa
kipindi cha mwaka mzima licha ya kupitiwa na mstari
wa 
Ikweta huku ukiwa ndio mlima
pekee uliosimama peke yake ukilinganisha

na milima mingine
duniani.


Mwisho.

NO COMMENTS