Ghana yaikomboa Afrika

0
391

Timu ya taifa ya Ghana Black Stars imeitoa Afrika kimaso maso Afrika aada ya kuifunga Marekani mabao 2-1 katika raundi ya pili ya kombe la dunia. 

Ilikuwa ni Ghana iliyokuwa ya kwanza kuuona mlango wa Marekani kupitia kwa Kevin Prince Boateng aliyepiga shuti kali la chini lililomshinda mlinda mlango wa Marekani Tim Howard na kushikilia usukani wa pambano hilo mapema. Lakini Marekani walipambana kufa na kupona mpaka mapumziko bado Ghana walikuwa wakiongoza.

Katika muda wa ziada ilikuwa ni Ghana waliotumia vizuri nafasi waliyoipata mapema katika dakika ya tatu tu mchezaji hatari Asamoah Gyan alipachika bao la pili na la ushindi.

Hadi mwisho wa muda wa ziada walikuwa ni Ghana waliotoka kifua mbele baada ya Marekani kushindwa kupata bao la kusawazisha sasa Ghana watakumbana na Uruguay ambao walikuwa wa kwanza kuingia robo fainali siku ya Jumamosi.

Jumamosi pia Uruguay ilipata tiketi ya kucheza  robo fainali hizo baada ya kuwafunga Korea Kusini mabao 2-1, mabao yote ya Uruguay yalifungwa na Luis Suarez na bao la Korea Kusini lilifungwa na Lee Chung Yong .

Michezo mingine ya raundi ya pili inaendelea  Jumapili ambapo katika mchezo wa kwanza siku Uingereza watapambana na Ujerumani na mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Argentina na Mexico huko Johanesburg. Katika michezo mingine ya raundi ya pili  Brazil watakumbana na Chile, Ureno watacheza na Hispania nao Uholanzi watapambana na Slovakia wakati Paraguay watapepetana na

Ghana yatamba
Mchezaji wa ghana John Pantsil akishangilia ushindi na bendera ya nchi yake.

 Japan.

NO COMMENTS