Hatimaye Ujerumani yajivua uteja kwa Italy

0
663

img_0156Baada ya kujaribu kwa takribani mara 9 hatimaye usiku wa leo timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kuwafunga Italy katika mashindano makubwa na kufanikiwa kusonga mbele hadi nusu fainali ya michuano ya Euro 2016.

Timu hizo zilikwenda sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na ilipofika hatua ya mikwaju ya penalti Ujerumani wakashinda 6-5

Miamba hiyo ya soka barani Ulaya ililazimika kwenda hadi penalti ya tisa ndipo mshindi alipopatikana kwa Italia kupoteza jumla ya penalti nne huku Ujerumani wakipoteza tatu.

Ujerumani walipata bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya penalti dakika ya 78.

Ujerumani walipata bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya penalti dakika ya 78.

Pia Ujerumani wameendelea kuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi kwa mikwaju ya penati kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita – historia inaonesha wamefanikiwa mikwaju mara 7 kati ya 8.
Shafi Dauda blog

NO COMMENTS