HATIMAYE MBUNGE GODBLESS LEMA APATA DHAMANA

0
606

Mbunge wa Jimbo la Arusha nchini Tanzania Godbless Lema aliyekuwa mahabusu kwa takribani miezi minne sasa baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uchochezi katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha amechiliwa kwa dhamana.

Dhamana ya mbunge huyo aliyekamatwa November 2 mwaka 2016 kwa kosa la uchochezi na kutoa lugha za kuudhi kwa viongozi wa serikali ya Tanania akiwemo Rais John Magufuli imetolewa Ijumaa katika Mahakama kuu kanda ya Arusha na Jaji wa Mahakama hiyo Mh. Salma Magimbi

Wakili anayemtetea mbunge huyo Peter Kibatala amesema baada ya kumaliza kazi ya kupatia mteja wake dhamana sasa wanajipanga kuanza kupambana na kesi ya msingi inayomkabili mteja wao ambayo hata hivyo haijajulikana ni lini itaanza kusikilizwa.Kusoma zaidi bofya

Akizungumza baada ya kupata dhamana mbunge huyo amesema kwa kipindi chote akiwa mahabusu amejionea mambo mengi ya ukiukwaji wa haki na kwamba ameandaa waraka anaotarajia kumfikishia rais John Magufuli.

Baada ya Mh.Lema kupata dhamana mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Freeman Mbowe amelalalilamikia jeshi la polisi kwa kuwazua wafuasi wa chama hicho kuingia kwenye viwanja vya mahakama huku akidai kuwa baadhi yao wamepigwa kitendo alichodai kuwa ni uonevu.

Katika mahakama hiyo walifurika Viongozi wa kitaifa chadema wakiongozwa na mawaziri wakuu wastaafu wawili Mh.Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, maprofesa wawili Abdalah Safari na Mwesiga Baregu , Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho na makamu wake , katibu mkuu, wabunge na watendaji mbalimbali.

CHADEMA ndio chama kikubwa cha upinzani nchini Tanzania ambacho tangu kuingia madarakani kwa rais wa awamu ya tano John Magufuli viongozi wake wamekuwa wakilalamika kuwa serikali inakandamiza uhuru wa vyama vya siasa.

NO COMMENTS