HARAMBEE YA MZEE EDDIS MGAWE DMV DOLA 3,000 ZAPATIKANA, WATANZANIA OKLAHOMA NAO WACHANGA JUMLA YA MICHANGO NI 13,1OO.

0
433

 Mary Mgawe(kuli) akiwa mwenye huzuni huku akilia kwa uchungu wa kufiwa na mpendwa baba yake marehemu mzee Eddis Mgawe aliyefariki siku ya Jumapili March 29, 2015 usiku , kushoto ni Jasmine Rubama akimfariji wakati wakiwa kwenye harambee iliyofanyika siku ya Jumatano na kuwezesha kukusanya jumla ya dola 3,000 na kufanya jumla ya fedha zilichangishwa wakiwemo wanaDMV na Watanzania Oklahoma kufikia dola 13,100 lengo lilikua 13,955 kiasi kilichobaki ni dola 855 Familia na kamati inatoa shukurani sana kwa moyo wenu na kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote.
Mama Jessica Mushala akiongoza maombi kabla ya kuanza kwa harambee iliyofanyika siku ya Jumatano April 1, 2015 Silver Spring, Maryland.

Da Tuma (kushoto) akiendesha mnada wa kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu mzee Eddis Mgawe unaotarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa April 3, 2015 kwenda Tanzania kwa mazishi.Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Said Mwamende akimsaidia Da Tuma kushika bidhaa zinazonadiwa na kukusanya fedha za manda kwa mdau atakayenunua chochote.

 Bwn. Said Mwamende akiwa ameshikilia kinyago pembeni ya meza iliyo na bidhaa vinavyopigwa mnada.
 Bwn. Sunday Shomari mmoja ya wanakamati akikusanya fedha kutoka kwa mwanaDMV aliyeweza kupiku wenzake na kujipatia kitenge.

Wanakamati watunza mahesabu wakifuatilia mnada.

Baadha ya WanaDMV waliojitokeza kwenye harambee.

 Baadhi ya wanaDMV waliohudhuria harambee. Wanne toka kushoto waliokaa mstari wa mbele ni Ben Mgawe mtoto wa marehemu.

NO COMMENTS