Dr.Bilal achangisha milioni 105 kuhifadhi vyanzo vya maji.

0
513
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo
Maalum, Mshauri wa kampuni ya VIP Engineering & Marketing, Fr. James Rugemalira,
wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika
Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na
Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro,
jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na OMR
Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewaomba wadau wa
maendeleo na uhifadhi wa mazingira kuisaidia taasisi ya Mfuko wa Udhamini wa
Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) ili kufanikisha uhifadhi wa vyanzo
vya maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme nchini.

Dk. Bilal aliyasema
hayo jana usiku wakati wa Chakula cha Hisani cha uchangiaji wa mfuko huo wa
EAMCEF katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam ambapo
alifanikiwa kuchangisha jumla ya Shs. 105.6 milioni.

“Napenda kuchukua
nafasi hii kuwaomba wadau wote: taasisi mbalimbali, sekta binafsi, wafanya
biashara na washirika wa maendeleo waendelee kuunga mkono uhudi hizi za
kuhifadhi misitu ya Milima yaTao la Mashariki kwa kutoa michango ya hali na
mali,” alisema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani. Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais alisema
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za
EAMCEF ili kuhakikisha kuwa misitu hiyo muhimu kitaifa na kimataifa inaendelea
kuchangia ustawi na uboreshaji wa maisha ya jamii na ukuaji wa uchumi wa taifa.
Aliwashukuru wadau
wote waliochangia katika hafla hiyo na kuwaomba “wadau wengine waige mfano huu
mzuri mliouonyesha jioni hii… napenda kuwaomba wale wote walioahidi kutimiza
ahadi zao kwani kwa kufanya hivyo mtasaidia kufanikisha mipango iliyokwisha
wekwa tayari.”
Katika chakula hicho
cha hisani, wadau waliochangia na kiasi cha fedha kikiwa kwenye mabano ni
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA (Shs. 5 milioni), Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (Shs. 10 milioni), Wakala wa Nishati Vijijini – REA (Shs. 6
milioni), Kampuni ya IPTL-PAP (Shs. 10 milioni), Songas (Shs. 13 milioni), VIP
Engineering & Marketing (Shs. 50 milioni) na waratibu wa shughuli hiyo
kampuni ya Regalia Media Consult ambayo imechangisha Shs. 1.2 milioni.
Aidha, katika
kufanikisha shughuli hiyo, kampuni ya Mabibo Beer, Wines and Spirits ilichangia
vinywaji vyenye thamani ya Shs. 2.1 milioni, ITV na Radio One walichangia
matangazo yenye thamani ya Shs. 640,000 na Hoteli ya Hyatt Regency walichangia
ukumbi na chakula vyote vikiwa na thamani ya Dola 3,000 (takriban Shs. 6.6
milioni).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa Mabibo Beer, Wines & Spirits na Mkurugenzi wa VIP Engineering Marketing Ltd, Benedicta Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPTL, Parthiban Chandrasakaran,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala wa REA, George Nchwale,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, pia
kulifanyika mnada wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jamii zinazozunguka
misitu hiyo ambazo zimenufaika na miradi ya kijamii inayofadhiliwa na EAMCEF
ambapo jumla ya Shs. 4.65 milioni zilikusanywa.
Awali, Mkurugenzi
Mtendaji wa EAMCEF, Francis Sabuni, alisema kwamba uhifadhi wa Misitu ya Milima
ya Tao la Mashariki ni muhimu kijamii, kitaifa na hata kimataifa kwani ndiko
kuliko na vyanzo vyote vya maji vinavyotegemewa na mabwawa makubwa matano
yanayozalisha umeme nchini Tanzania ambayo ni Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya
Mungu, Hale na Pangani.
Sabuni alisema, Milima
ya Tao la Mashariki ina eneo la ardhi lenye ukubwa wa takriban kilometa za
mraba 5,350 ambalo liko kwenye wilaya 15 ndani ya mikoa mitano.
“Mkoa wa Kilimanjaro
kuna Milima ya Upare Kaskazini na Kusini iliyoko katika wilaya za Mwanga na
Same; Mkoa wa Tanga kuna Milima ya Usambara Magharibi na Mashariki pamoja na
Milima ya Nguu katika wilaya za Lushoto, Korogwe, Muheza, Mkinga na Kilindi na
Mkoa wa Dodoma kuna wilaya ya Mpwapwa iliko Milima ya Rubeho,” alisema.
Mikoa mingine ni
Morogoro ambako kuna Milima ya Nguru, Uluguru, Ukaguru, Udzungwa, Malundwe,
Mahenge na Rubeho ambayo iko katika wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa,
Kilombero, Ulanga na Manispaa ya Morogoro, pamoja na Mkoa wa Iringa wenye
Milima ya Udzungwa iliyoko kwenye wilaya za Kilolo na Mufindi.
Kwa mujibu wa Sabuni,
Milima ya Tao la Mashariki inaunda ukanda wa milima uliopo Mashariki mwa Afrika
ambao unatambuliwa duniani kama moja ya maeneo 34 yenye utajiri mkubwa wa
bioanuwai na kwa kuwa na viumbe ndwele wengi wanaokabiliwa na tishio la
kutoweka.
Bioanuwai ya
milimahiyo inatajwa kuwa na manufaa makubwa kijamii katika kupunguza athari za
umaskini ambapo mazao ya misitu kama kuni, mbao, madawa ya asili, matunda pori
na aina nyingine za vyakula yanakadiriwa kuchangia takriban asilimia 40 ya
mahitaji yote ya kaya katika baadhi ya jamii zinazopakana na milima hiyo.
Misitu ya milima hiyo
ndiyo vyanzo vikuu pia vya maji ambavyo kwa ujumla hutoa maji kwa matumizi ya
viwanda vikubwa nchini pamoja na baadhi ya wananchi wanaokadiriwa kufikia
asilimia 25 ya Watanzania wote wanaoishi katika miji ya Iringa, Kilolo,
Mufindi, Mpwapwa, Morogoro, Kilosa, Gairo, Mvomero, Mahenge, Ifakara, Muheza,
Chalinze, Korogwe, Lushoto, Mwanga, Same, Soni, Mikumi, Kilindi, Handeni,
Kibaha pamoja na majiji ya Tanga na Dar es Salaam.
Uzalishaji wa umeme
nchini Tanzania unategemea zaidi ustawi wa milima hiyo kwani maji yanayopatikana
huko ndiyo hutumika kuzalisha asilimia 90 ya nishati hiyo inayotumia nguvu za
maji, ambapo inakadiriwa kwamba asilimia 50 ya umeme wote unaotumika nchini
Tanzania huzalishwa katika mabwawa hayo matano yaliyotajwa.
Sabuni anasema, kwa
sababu ya kuwa na ardhi yenye rutuba pamoja na mvua za kutosha, milima hiyo ni
maarufu kwa kilimo kikubwa cha mpunga, miwa, chai, na kahawa na hivyo kusaidia
kwa kiasi kikubwa katika kufikiwa kwa malengo ya mikakati ya Serikali ya Kilimo
Kwanza, SAGCOT na Matokeo Makubwa Sasa (BRN), huku pia ikiwa kivutio kikubwa
cha utalii kutokana na kuwa na viumbe ndwele wengi.
“Mto Ruvu ndicho
chanzo kikubwa cha maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine, lakini
chanzo chake ni Milima ya Uluguru mkoani Morogoro, hivyo bila kuilinda Dar es
Salaam itakosa maji na hivyo kuikosesha Tanzania asilimia zaidi ya 70 ya pato
lake la taifa kwani maji ya mto huo mbali ya kutumiwa na wanajamii kwa shughuli
mbalimbali, lakini pia hutumika viwandani kwa uzalishaji mkubwa wa bidhaa,”
anasema Sabuni.
Hata hivyo, inaelezwa
kwamba, katika kipindi cha miaka 200 iliyopita, asilimia 70 ya misitu ya Milima
ya Tao la Mashariki ilitoweka na kama hali hiyo haitadhibitiwa, kiasi cha
misitu kilichobaki kinaweza kutoweka kabisa katika miaka 20 ijayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwakilishi wa ITV na Radio One, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 

Katika kukabiliana na
tishio hilo, EAMCEF inashirikisha jamii zinazoizunguka misitu hiyo katika
uhifadhi ambapo hutenga asilimia 50 ya rasilimali zake za ufadhili kwa ajili ya
miradi ya maendeleo ya kijamii.
“Mfuko unafadhili
miradi mbalimbali kwenye Halmashauri za Wilaya 11 ikilenga misitu 9 ya Hifadhi
za Mazingira Asilia za Chome na Magamba (Same, Lushoto, Korogwe); Hifadhi za
Mazingira Asili za Amani na Nilo (Korogwe, Muheza, Mkinga); Hifadhi za
Mazingira Asili za Uluguru na Mkingu (Morogoro Manispaa, Morogoro na Mvomero);
Hifadhi za Mazingira Asili za Udzungwa Scaep (Kilombero) na Hifadhi ya Taifa ya
Milima ya Udzungwa (Mufindi, Kilolo na Kilombero),” anafafanua Sabuni.
Sabuni alieleza
kwamba, tangu kuanzishwa kwake, EAMCEF imefadhili zaidi ya miradi 200 yenye
thamani ya zaidi ya Shs.3.4bilioni ambapo miti zaidi ya milioni 18 imepandwa
katika hekta zaidi ya 10,000 kwenye maeneo mbalimbali ya milima hiyo.
“Miradi hiyo katika
vijiji zaidi ya 130 ni pamoja na ufugaji wa mbuzi wa maziwa zaidi ya 250, ng’ombe
wa maziwa zaidi ya 30, kuku zaidi ya 1,000, nguruwe zaidi ya 100, ufugaji nyuki
zaidi ya mizinga ya kisasa 800, majiko banifu zaidi ya 5,000, uwekaji na
uimarishaji wa mipaka ya misitu ya hifadhi zaidi ya kilometa 2,000 na
kadhalika,” anasema Sabuni.
Naye Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini ya EAMCEF, Profesa Gerald Monela, aliishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kubuni na kuanzisha mfuko huo, kwani kulinda
bioanwai zilizoko kwenye misitu ya milioma hiyo ni muhimu zaidi.
“Bioanwai zinazopatika
kwenye misitu hii ni adimu na hazipatikani sehemu nyingine duniani, lakini
misitu hii ni muhimu kwa upatikanaji wa maji, hivyo ni muhimu sana kuitunza na
kuilinda,” alisema.
Profesa Monela
aliwashukuru wadau wote waliochangia na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili
kuunga mkono uhifadhi wa misitu hiyo muhimu kwa ustawi wa jamii na taifa kwa
ujumla.

NO COMMENTS