Diamond , Vanessa na Ommy D watamba tuzo za Afrimma

0
958

TUZODiamond akiwakazidiwa na furaha.
12145300_972400302833337_664949009_nVanessa Mdee.
Hii ndio orodha ya washindi.

Best Male (South Africa) – AKA
Best Male (East Africa) – Diamond Platnumz
Best Male (Central Africa) – Yuri Da Cunha
Best Male (West Africa) – Davido
Best Female (East Africa) – Vanessa Mdee
Best Female (West Africa) – Yemi Alade
AFRIMMA Inspirational Song – Bracket feat. Tiwa Savage and Diamond Platnumz for ‘Alive’
Best DJ (US) – DJ Simplesimon
Best Newcomer – Ommy Dimpoz
Best Collaboration – AKA feat. Da Les and Burna Boy for ‘All Eyes on Me’
Best Dance Video – Diamond Platnumz for ‘Nana’
Best Video – Wizkid for ‘Ojuelegba’
Artist of the Year – Diamond Platnumz
Legendary Award – Yossou N’Dou

Inaweza ikawa siyo mara ya kwanza kwa msanii Diamond Platnumz kuchukua tuzo mbalimbali za kimataifa lakini kwa Vanessa Mdee inaweza ikawa moja kati ya historia nzuri kwake huku Ommy Dimpoz akiwa na kila sababu ya kufurahia tuzo yake ya kwanza ya kimataifa baada ya kujinyakulia tuzo maarufu za Afrimma.Kusoma zaidi

Wasanii hao walijinyakulia tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best Inspirational Song of The Year.

Wakati huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.

Washindi wengine wa tuzo hizo katika vipengele tofautitofauti kutoka nchi mbalimbali ni kama vile; God Father, AKA, Yemi Alade, Davido, Wizkid na Yuri.

Picha na habari kwa hisani ya GPL

NO COMMENTS